1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa Fatah warudishwa Gaza

3 Agosti 2008

Gaza:

Kiasi ya wafuasi 30 wa chama cha wapalestina cha FATAH waliokimbilia Israel baada ya mapigano makali dhidi ya wanajeshi wa Hamas katika ukanda wa Gaza, wamerudishwa katika eneo hilo, baada ya kukamatwa kwa muda mfupi na wanajeshi wa Israel.

Wafuasi hao wa FATAH walikua miongoni mwa wafuasi 180 wa kundi hilo linalomuunga mkono rais Mahmoud Abbas na ambao walipewa hufadhi nchini Israel jana, baada ya wapalestina 9 kuuawa na wengine 95 kujeruhiwa, pale Hamas waliposhambulia eneo lao karibu na mji wa Gaza. Msemaji wa Hamas Sami Abu Zuhri amesema watu kadhaa walioukimbia ukanda wa Gaza wemerudi na kutiwa nguvuni. Hamas waliwashinda nguvu wapiganaji wa Fatah katika mapigano makali mwaka jana na kutwaa mamlaka ya eneo hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW