1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wafuasi wa Imran Khan waandamana kushinikiza aachiwe

25 Novemba 2024

Mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu wa zamani wa Pakistan Imran Khan wamefanya maandamano kushinikiza kuachiliwa kwa kiongozi huyo aliyefungwa jela.

Wafuasi wa Imran Khan wakiandamana kushinikiza kiongozi huyo wa zamani aachiwe huru.
Wafuasi wa Imran Khan wakiandamana kushinikiza kiongozi huyo wa zamani aachiwe huru. Picha: Muhammad Sajjad/AP Photo/picture alliance

Waandamanaji hao wamefika hadi pembezoni mwa mji mkuu wa Islamabad huku kukiwa na ripoti za kutokea ghasia katika maeneo mengine.

Mamlaka zimeimarisha usalama huku barabara zinazoingia mji mkuu zikifungwa ili kuwazuia waandamanaji ambao Khan amewataka kuandamana hadi bungeni.

Maafisa na mashuhuda wamesema usafiri wa umma umetatizika huku vituo vya mabasi vikifungwa katika mkoa wa Punjab ili kuzuia waandamanaji wanaongozwa na wanachama wa chama cha Khan cha Tehreek-e-Insaf PTI.

Waziri wa habari wa jimbo la Punjab Uzma Bukhari amesema hawataruhusu waandamanaji kuuvamia mji mkuu na kwamba wafuasi 80 wa Khan tayari wamekamatwa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW