1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafuasi wa Kabila waunda muungano

Sekione Kitojo
2 Julai 2018

Wanasiasa na wanaharakati wanaomuunga mkono Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameunda kile wanachokiita kuwa ni "Jukwaa la Uchaguzi" miezi michache kabla ya uchaguzi mkuu.

DR Kongo Kampagne für Präsident Joseph Kabila
Picha: DW/K. Tiassou

Wapiga kampeni wa kumuunga Rais Kabila, ambaye wakosoaji wanamshutumu kwa kutaka kuwania muhula wa tatu kinyume na sheria, walianzisha kundi hilo siku ya Jumapili (Julai 1) bila ya kusema iwapo atagombea katika uchaguzi huo muhumu mwaka huu.

Hatua hiyo inakuja huku kukiwa na uvumi mkali kuhusiana na iwapo Kabila, ambaye amekuwapo madarakani tangu mwaka 2001, atawania muhula mwingine katika uchaguzi ambao umeahirishwa mara mbili  hapo Desemba 23.

Kundi hilo linalojulikana kama Common Front for Congo (FCC), ambalo limemtaja Kabila kuwa mwenye "mamlaka  ya  kiroho", linataka kukamata madaraka kwa njia ya kidemokrasia kwa kumuunga mkono mgombea pekee katika uchaguzi wa rais kwa misingi ya mpango wa pamoja, kwa mujibu wa mkuu wa ofisi ya rais, Nehemiah Mwilanya Wilondja.

Hata hivyo, Kabila hajaweka wazi nia yake licha ya miito kutoka Marekani, Ufaransa na Uingereza kumtaka atangaze wazi kwamba hatagombea tena.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW