Wafuasi wa rais wa zamani na wa sasa wapambana Bolivia
23 Septemba 2024Matangazo
Waandamanaji hao walirushiana mawe na mabomu ya kienyeji hapo jana, huku polisi wakiwapuliza gesi ya machozi. Watu wanane wamejeruhiwa, kwa mujibu wa wizara ya afya ya Bolivia.
Makabiliano hayo yametokea wakati maelfu ya wafuasi wa Morales wakiendelea na safari yao ya kilomita 190 wiki nzima kuelekea mji mkuu, La Paz, kupinga siasa za uhasama wakati taifa hilo la Andean likielekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Morales na aliyekuwa waziri wake wa uchumi na kugeuka hasimu wake, rais wa sasa Luis Arce, wanawania kukiongoza chama tawala cha kisoshalisti, MAS, kuelekea mwaka 2025.