Wafuasi wa upinzani na serikali waandamana Venezuela
18 Agosti 2024Wananchi wa Venezuela katika mataifa mbalimbali ulimwenguni waliingia mitaani wakiwa na bendera za taifa lao kuitikia wito kutoka kwa chama cha upinzani nchini humo wa kutetea madai ya ushindi katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo wa mwezi uliopita na wenye utata, ambao Rais Nicolás Maduro alitangazwa mshindi.
Maandamano hayo yamefanyika katika miji kadhaa duniani ikiwemo ya Tokyo, Sydney, Mexico City na mengine kadhaa kusisistiza kwamba upinzani ndio ulioshinda katika uchaguzi nchini humo.
Soma zaidi. Wafuasi wa upinzani na serikali kuandamana Venezuela
Huku maelfu ya Wavenezuela wakipeperusha bendera ya taifa, kiongozi wa upinzani, María Corina Machado, aliungana na waaandamanji katika mitaa ya jiji la Caracas huku sauti za watu zikisikika zikisema kwamba kila kura iheshimiwe na ulimwengu utambue kuwa "rais mteule ni Edmundo González."
Upinzani nchini Venezuela umeendelea kutoa wito kwa jumuiya ya kimatiafa kumshinikiza Maduro kukubali kuwa alishindwa katika uchaguzi mkuu.