Wafungwa 12 wafa kutokana na kipindupindu Kamituga
22 Desemba 2022Matangazo
Mbali na waliofariki, hospitali ya Kamituga imewapokea wafungwa wengine 31 walioambukizwa ugonjwa huo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema licha ya hali hiyo ya magonjwa inayoendelea, wafungwa wanaendelea pia kukosa chakula, hali ambayo inaweza kudhoofisha afya zao zaidi.
Waziri wa Afya katika jimbo la Kivu Kusini Masine Kinenwa amesema kwa sasa juhudi zinafanyika ili kudhibiti kipindupindu kwenye eneo hilo.
Kinenwa amesema kuna ujumbe wa madaktari toka idara ya afya umeelekea Kamituga ukiambatana na madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, maafisa wa Shirika la Afya Duniani, WHO, pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia Watoto, UNICEF, katika juhudi za kujaribu kuudhibiti ugonjwa huo.