1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wafungwa na walinzi wauawa katika gereza la Mogadishu

13 Julai 2024

Wafungwa watano na walinzi watatu wameuawa katika majibizano ya risasi wakati wa jaribio la kutaka kutoroka katika gereza kuu katika mji mkuu Mogadishu. Wafungwa hao wanadaiwa kuwa ni wanachama wa Al-Shabaab

Somalia / Mogadischu
Wanajeshi wa Somalia wakiwa kwenye doria katika mitaa ya MogadishuPicha: Farah Abdi Warsameh/AP Photo/picture alliance

Wafungwa watano wanaosemekana kuwa ni wanachama wa kundi wa wanamgambo la Al-Shabaab nchini Somalia na walinzi watatu wameuawa katika majibizano ya risasi wakati wa jaribio la kutaka kutoroka katika gereza kuu katika mji mkuu Mogadishu. Hayo yamesemwa na wakuu wa magereza na mashuhuda wa tukio hilo.

Soma zaidi. Nchi hasimu za Somalia na Ethiopia zafanya mazungumzo Uturuki

Al-Shabaab imekuwa ikifanya mashambulizi mengi ya mabomu na mashambulizi mjini Mogadishu na maeneo mengine ya nchi hiyo yenye machafuko, ingawa ni machache yamerekodiwa katika miezi ya hivi karibuni.

Serikali ya Somalia imeungana na wanamgambo wa koo za ndani kupambana na wanamgambo hao wa Kiislamu katika kampeni yake inayoungwa mkono na jeshi la Umoja wa Afrika pamoja na mashambulizi ya kutokea angani ya jeshi la Marekani ingawa mapambano yao yamekabiliwa na vikwazo vya kundi la Al-Shabaab ambalo mapema mwaka huu lilidai kuchukua udhibiti wa maeneo mengi katikati mwa nchi hiyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW