Wafungwa wateswa kinyama Guantanamo
27 Juni 2023Matangazo
Kwenye ripoti yao waliyoiwasilisha siku ya Jumatatu (Juni 26), wataalamu hao wamesema mazingira ya wafungwa 30 wa mwisho katika gereza hilo ni ya kikatili, kinyama na udhalilishaji.
Mwandishi maalumu wa Umoja wa Mataifa, Fionnuala Ni Aolain, alisema dhuluma katika gereza hilo ni sawa na ukiukwaji wa haki za kimsingi na uhuru wa wafungwa.
Wafungwa hao wanashikiliwa kwa takriban miongo miwili baada ya kukamatwa kama washukiwa kufuatia mashambulizi ya al-Qaida nchini Marekani mwaka wa 2001.
Wataalamu wa Umoja wa Mataifa walilitembelea gereza la Guantanamo mnamo mwezi Februari.