1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Waganda watoa heshima za mwisho kwa mwanariadha Cheptegei

14 Septemba 2024

Raia wa Uganda wametoa heshima zao za mwisho kwa Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyefariki baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake wa zamani.

Waganda watoa heshima za mwisho kwa mwanariadha Cheptegei
Waganda watoa heshima za mwisho kwa mwanariadha CheptegeiPicha: Hajarah Nalwadda/AP/picture alliance

Raia wa Uganda Jumamosi ya leo wametoa heshima zao za mwisho kwa Mwanariadha Rebecca Cheptegei aliyefariki baada ya kumwagiwa petroli na kuchomwa moto na mpenzi wake wa zamani.

Mwanariadha huyo wa mbio za marathon mwenye umri wa miaka 33, alikuwa ameshiriki katika Michezo ya Olimpiki ya Paris ya hivi majuzi. 

Soma zaidi.Mwanariadha wa olimpiki wa Uganda afariki baada ya shambulizi la moto 

Shambulio hilo la kikatili lilishtua ukanda mzima mashariki mwa Afrika na kuibua hisia kali duniani kote, huku wanaharakati wakilaani kitendo hicho cha unyanyasaji wa kijinsia kilichotokea nchini Kenya.

Mapema leo, wakaazi, maafisa na jamaa walipanga foleni ili kutoa heshima zao katika kijiji cha Bukwo, karibu kilomita 380 kaskazini mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW