1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wageni wanaikimbia Haiti

21 Februari 2004
PORT-AU-PRINCE: Nchini Haiti kuendelea kupamba moto vita vya ndani vya umwagaji damu kumewafanya wageni wengi waihame nchi. Wamarekani, Wafaransa na Wakanada miya kadha wamekusanyika uwanja wa ndege wa mji mkuu kwa shabaha ya kuihama Haiti. Katibu Mkuu wa UM Kofi Annan karibuni anataka kumteua mjumbe wake maalumu wa maswali ya Haiti. Katika mji mkuu Port-Au-Prince yalipamba moto tena mapigano kati ya wafuasi na wapinzani wa Rais mtawala Jean-Bertrand Aristide. Katika mkutano wa maandamano wapinzani wake walidai kuwa Rais Aristide ajiuzulu. Watu wawili walipigwa risasi na kuuawa na wengine 20 walijeruhiwa katika mapigano hayo kwenye mji mkuu Port-Au-Prince, kiliarifu Chama cha Msalaba Mwekundu. Wanadiplomasia wa nchi kadha wamemkabidhi Rais Aristide mpango wa amani unaoshauri kuwa wanamgambo wa kiasi wapokonywe silaha na ateuliwe Waziri Mkuu mpya mwenye madaraka makubwa zaidi. Hata hivyo, mpango huo hauna nafasi nzuri za kufanikiwa kwa sababu hautoi mwito wa kujiuzulu Rais Aristide. Annan amteuwa mjumbe maalumu wa haki za binadamu:
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW