1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiganaji wa Wagner waendelea kujiimarisha Bakhmut

6 Mei 2023

Jeshi la Ukraine jana lilipuuzilia mbali vitisho vya kiongozi wa kampuni ya mamluki wa kijeshi ya Urusi ya Wagner, Yevgeny Prigozhin, aliyedai kuwaondoa wanajeshi wake katika mji unaozozaniwa wa Bakhmut wiki ijayo

Russland Yevgeny Prigozhin
Picha: Yulia Morozova/REUTERS

Mwakilishi wa shirika la kiintelijensia la Ukraine Andriy Chernyak ameliambia shirika la habari la nchini humo la RBK kwamba jeshi halijaona dalili yoyote ya mamluki hao kuondoka na kuongeza kuwa matamshi hayo yanatokana na ukweli kwamba Prigozhin hataweza kutimiza ahadi yake ya kuukamata mji huo ifikapo Mei 9.

Soma zaidi: Mmiliki wa Wagner: Vita nchini Ukraine vinaweza kudumu kwa miaka kadhaa

Jana Ijumaa alisema wanajeshi wake watajiondoa Jumatano ijayo, huku akilishutumu jeshi la Urusi kwa kile alichosema kuwanyima watu wa Urusi ushindi. 

Msemaji wa ikulu ya Kremlin Dmitri Peskov amesema hawezi kulizungumzia suala hilo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW