1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaJamhuri ya Kongo

Wagombea 24 wa Urais Kongo warejesha fomu

Jean Noël Ba-Mweze
9 Oktoba 2023

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, ilimaliza jana Jumapili kupokea fomu za wagombea urais kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Desemba 20.

Makao Makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo CENI
Makao Makuu ya Tume Huru ya Uchaguzi Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo CENIPicha: Dirke Köpp/DW

Jumla wagombea 24 ndio waliorejesha fomu zao kwenye ofisi ya kupokea na kushughulikia maombi hayo.

Kila mmoja wao alilipa dhamana ya dola 64,000 za Kimarekani ambazo hazitarejeshwa.

Orodha rasmi itatangazwa baada ya uchunguzi wa kina kufanywa na CENI pamoja na Mahakama ya Kikatiba. 

Miongoni mwa wagombea hao ni kwanza Rais Félix Tshisekedi ambaye atawania muhula wa pili kwa niaba ya Union sacrée de la nation ambayo ni muungano wa vyama vinavyomuunga mkono.

Tshisekedi ambaye ni mzaliwa wa Kasaï alionya dhidi ya wale aliowataja kuwa wagombea wa wageni ambao alisema watakuja na matamshi kutoka ugenini.

Soma pia:Wagombea 24 nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo wametangaza rasmi kuwa watagombea urais katika uchaguzi wa Desemba

Alisema Matamshi kama dhana ya jinsia. Nchini Kongo hatuna tatizo la mwelekeo wa kijinsia.

"Mtawatambua watu hao watapokea amri kutoka ugenini ili  kujumuika pamoja kwa nia ya kuwa na nguvu zaidi."

Tshisekedi hakutaja jina lolote, lakini wapo wengi Wakongo wanaoamini kwamba amemlenga Daktari Denis Mukwege, mgombea wa kibinafsi anayeungwa mkono hasa na wanawake pamoja na wasomi.

Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel ya mwaka 2018, ambaye ni daktari wa magonjwa ya wanawake, ndiye mwanzilishi wa hospitali ya Panzi inayotibu wanawake waliobakwa pamoja na wahasiriwa wengine wa ukatili mashariki mwa Kongo. Mukwege ni mzaliwa wa Kivu kusini.

Upinzanimkali unaomkabili Tshisekedi

Upinzani mwingine unaomkabili Tshisekedi ni ule wa mfanyabiashara Moïse Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa Katanga ambaye pia ni kiongozi wa chama Ensemble pour la République.

Wafuasi wa Felix Tshisekedi wakiwa katika mkutano wa kisiasaPicha: Justin Makangara/REUTERS

Katumbi ni mzaliwa wa Katanga lakini uraia wake uko mashakani. Pia kuna Waziri Mkuu wa zamani Augustin Matata Ponyo, seneta ambaye pia ni kiongozi wa LGD. Anashitakiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma.

Upande wake Martin Fayulu, kiongozi wa chama ECIDÉ akiwa pia mratibu wa muungano wa Lamuka tayari amerejea baada ya kutokubali kwamba alishindwa uchaguzi wa mwaka 2018.

Soma pia:Mukwege akosoa matayarisho uchaguzi DRC

Mzaliwa huyo wa Kwilu bado ana mashaka kuhusu uchaguzi kufanyika mwaka huu:

"Je, una uhakika kutakuwa na uchaguzi Desemba 20 ? Mimi sina uhakika. Je, tuko katika mchakato unaoaminika ? Idadi kamili ya wapiga kura ni gani ?"

Miongoni mwa wagombea 24 waliorejesha fomu zao kuna  mwanamke mmoja tu. Marie-José Ifoku, kiongozi wa chama AENC ambaye aligombea tena urais mwaka 2018.

Vyama vya siasa vya upinzani Afrika vimetekeleza wajibu wao?

02:19

This browser does not support the video element.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW