1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea 26 kuwania kiti cha urais Kongo

5 Novemba 2023

Tume huru ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, CENI, imewasajili rasmi wagombea 26 kwa ajili ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Disemba.

Rais Felix Tshisekedi, Moise Katumbi, Denis Mukwege na Martin Fayulu miongoni mwa wagombea wa uchaguzi wa Desemba 20 nchini Kongo
Rais Felix Tshisekedi, Moise Katumbi, Denis Mukwege na Martin Fayulu miongoni mwa wagombea wa uchaguzi wa Desemba 20 nchini KongoPicha: AFP/Getty Images, picture alliance, G. Kusema, DW

Mahasimu wa zamani, wagombea wa mara ya kwanza, na wagombea wa urais waliowekwa kando katika chaguzi zilizopita ni miongoni mwa wanaogombea safari hii kushindana na rais Felix Tshisekedi anaetetea kiti chake.

Wachambuzi wanasema wanaogombea ni wengi na hii inaweza kutoa ushindani na mpasuko ndani ya makundi ya upinzani na kuiongeza nafasi ya Tshisekedi kuchukua ushindi na kuongoza nchi hiyo katika muhula mwengine wa pili.

Miongoni mwa wapinzani wa kuu wa Tshisekedi ni pamoja na mshindi wa amani ya Nobel Denis Mukwege, gavana wa zamani wa mkoa wa utajiri wa madini wa Katanga Moise Katumbi, na aliyemaliza wa pili katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2018 Martin Fayulu.