1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea umakamu rais Marekani washiriki mdahalo

2 Oktoba 2024

Wagombea wa umakamu wa rais nchini Marekani, Tim Walz na JD Vance, wamepambana katika mdahalo wa televisheni uliogubikwa na masuala mazito kuanzia mzozo wa Mashariki ya Kati hadi huduma za utoaji mimba nchini humo.

JD Vance, Tim Walz
Wagombea wa umakamu wa urais wa Marekani, Tim Walz na JD Vance.Picha: Matt Rourke/AP/picture alliance

Mdahalo huo ulifunguliwa na swali kuhusu Mashariki ya Kati, wakati wasiwasi unaongezeka kwamba ukanda huo unakaribia kuingia kwenye vita kamili.

Mgombea wa chama cha Democratic, Tim Walz alisema Marekani inahitaji kuwepo kwenye ukanda huo na anaiunga mkono Israel dhidi ya makundi aliyodai yanasaidiwa na Iran, akimkosoa mgombea wa urais kupitia chama cha Republican, Donald Trump, kwa kuwa kigeugeu.

Soma zaidi: Trump asema kuna vitisho vikubwa dhidi ya maisha yake kutoka Iran

"Tukumbuke hili lilianzia wapi. Oktoba 7, magaidi wa Hamas, waliwaua zaidi ya Waisraeli 1,400 na kuchukua wafungwa. Uwezo wa Israel kujilinda ni jambo la msingi sana, kuwarejesha mateka na kukomesha mzozo wa kibinadamu huko Gaza. Lakini ni muhimu pia kwa Israel na washirika kujiimarisha, kwa Marekani kuwa na uongozi thabiti huko. Hili liko wazi.'' Alisema Walz.

Vance, kwa upande wake, alimtetea Trump akisema ndiye aliyeufanya ulimwengu kuwa salama zaidi alipokuwa madarakani. 

Aidha, wawili hao walivutana juu ya suala la uaviaji mimba, ambalo mgombea wa urais, Kamala Harris, analipigia upatu kwenye kampeni zake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW