Wagombea urais Kongo wataka kuzuiwa wizi wa kura
31 Oktoba 2023Matangazo
Katika taarifa ya pamoja, wagombea hao wameahidi kushirikiana ili kuepusha kile walichosema ni "uchakachuaji wowote wa matokeo" huku wakiita Tume ya Uchaguzi (CENI) kuchukuwa hatua kdhaa, ikiwemo kuchapishwa kwa orodha za wagombea na kuweka wazi ramani ya vituo vyote vya kupigia kura.
Soma zaidi: Wafuasi wa Katumbi waridhishwa kuruhusiwa kuwania urais DRC
Wagombea wote wa upinzani wameelezea wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuwepo udanganyifu na ukosefu wa uwazi katika uchaguzi.
Wagombea hao ni pamoja na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Denis Mukwege, gavana wa zamani wa mkoa wa utajiri wa madini wa Katanga, Moise Katumbi, na mwanasiasa aliyeshika nafasi ya pili katika uchaguzi wa rais mwaka wa 2018, Martin Fayulu.