1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Wagombea urais Senegal waanza kampeini za uchaguzi

9 Machi 2024

Wagombea urais nchini Senegal wameanza kampeni zao za uchaguzi leo kufuatia wiki za vurugu kote nchini humo baada ya kucheleweshwa kwa uchaguzi huo

Maandamano ya kupinga kuahirishwa uchaguzi katika mji wa Dakar nchini Senegal mnamo Machi 2, 2024
Maandamano ya kupinga kuahirishwa uchaguzi Senegal Picha: Cem Ozde/Anadolu/picture alliance

Wagombea 19 walioidhinishwa kushiriki kinyang'anyiro hicho, sasa wana muda mfupi wa kuwashawishi wapiga kura kabla ya uchaguzi huo uliopangiwa sasa kufanyika Machi 24.

Soma pia: Muswada wa maridhiano waridhiwa Senegal

Kampeni na kMuswada wa maridhiano waridhiwa Senegalura hiyo ya urais vyote vitafanyika katika mwezi mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza kesho Jumapili kwa kutegemea kuonekana kwa mwezi .

Uchaguzi uliahirishwa mwezi uliopita

Mwezi uliopita, Rais Macky Sall, ambaye haruhusiwi kugombea tena kutokana na ukomo wa mihula, aliahirisha uchaguzi huo wiki chache kabla ya tarehe iliyopangwa ya Februari 25.

Soma pia: Senegal: Rais Sall asema ataachia madaraka muda wake ukifika

Baraza la katiba nchini Senegal lilipinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo na kuiagiza serikali kuweka tarehe mpya haraka iwezekanavyo.

Mapema wiki hii, msemaji wa serikali Abdou Karim Fofana alitangaza tarehe hiyo mpya ya Machi 24.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW