Wagombea Urais Taiwan wachuana katika mdahalo
30 Desemba 2023Mdahalo huo unajiri karibu wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Januari 13, 2024 na unaofuatiliwa kwa karibu na Washington na Beijing.
Wagombea hao walipambana katika mjadala uliorushwa moja kwa moja kwenye runinga na mgombea wa chama kilichopo madarakani cha Democratic Progressive Party (DPP) ambaye pia ni Makamu wa rais Lai Ching-te, ametetea sera ya chama chake cha ya kutaka uhuru wao kutoka kwa China.
Wapinzani wake walimshambulia mara kwa mara, wakisema kuwa matamshi yake ya kuunga mkono uhuru "yatadhoofisha usalama wa Taiwan".
China inadai kuwa kisiwa cha Taiwan ni sehemu ya himaya yake, na imeapa kutumia mabavu kukidhibiti ikiwa italazimika, na ilisitisha mawasiliano ya ngazi za juu na Rais wa sasa wa Taiwan Tsai Ing-wen.