Wagombea urais Tunisia walalamikia vitisho
2 Agosti 2024Matangazo
Huku muda wa mwisho wa kujiandikisha katika kinyang'anyiro cha kugombea urais ukikaribia hapo Agosti 6, wanasiasa 11 wa upinzani wanaotarajia kushindana na Saied, wametoa taarifa ya pamoja wakizilaani mamlaka nchini humo. Kati ya wagombea hao 11, hakuna hata mmoja kati yao ambaye amepokea cheti cha kuonyesha kwamba hawajahusika katika uhalifu wa aina yoyote ile, hilo likiwa ni sharti jipya litakalowapa fursa ya kusonga mbele katika hatua ya kujisajili. Msemaji wa tume ya uchaguzi nchini humo amesema wizara ya usalama wa ndani itawasiliana na wagombea hao na kuwapa vyeti hivyo ingawa hakusema ni lini hilo litakapofanyika. Saied alitaganza Julai 19 kwamba atawania muhula mwengine wa urais.