1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagombea wa uenyekiti wa tume ya AU washiriki katika mdahalo

14 Desemba 2024

Mdahalo wa maswali na majibu kwa wagombea wa nafasi ya uwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika kwa jina Mjadala Afrika, ulifanyika Ijumaa katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika, Moussa Faki Mahamat Picha: Giscard Kusema/Press Office Presidency of DRC

Wakati wa mdahalo huo uliodumu kwa masaa mawili, wagombea hao watatu ambao ni waziri mkuu wa zamani wa Kenya Raila Odinga, waziri wa mambo ya nje wa Djibouti  Mahamoud Ali Youssouf na Richard Randriamandrato, aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Madagascar,  walielezea mipango yao ya usalama wa kikanda wakati kukishuhudiwa migogoro na mapinduzi ya kisiasa barani Afrika.

Wagombea hao pia walishinikiza kuwepo kwa biashara baina ya mataifa ya Afrika pamoja na masuala mengine.

Afrika inataka viti viwili vya kudumu katika baraza la usalama la UN

Wagombea wote walitoa wito wa kuwepo kwa viti viwili vya kudumu kwa nchi za Kiafrika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kuliwakilisha kwa ufanisi bara hilo .

Odinga alisema kuwa viti viwili vya kudumu vyenye kura ya turufu ni lazima kwa Afrika na kwamba hatua hiyo ni ya haki kwasababu bara hilo lina zaidi ya mataifa 50.

Mahamat rais mpya wa halmashauri kuu ya AU

Wakati huo huo, Randriamandrato aliyahimiza mataifa wanachama wa Umoja huo wa Afrika, kutumia fursa hiyo na kuchagua kwa kauli moja atakayeiwakilisha Afrika katika Baraza hilo la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Randriamandrato pia alizihimiza nchi hizo kuchukua udhibiti wa usalama wao wa ndani huku akionya kwamba kambi za kijeshi za kigeni zinapaswa kuwa suala la zamani kwa sababu zinaweza kuwa chanzo cha migogoro.

Umoja wa Afrika wajadili matatizo ya bara hilo

Kwa upande wake, Youssouf alisema kwamba usalama wa kikanda unaweza kuimarishwa ikiwa rasilimali kwa ajili ya kikosi cha kikanda kitakachokuwa katika hali ya tahadhari zitaongezwa ili kupunguza utegemezi zaidi wa ushirikiano wa mataifa ya nje kwa rasilimali.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Madagascar Richard RandriamandratoPicha: JONATHAN HORDLE/AFP

Youssouf ameongeza kuwa ikiwa hakuna umoja wa maslahi miongoni mwa mataifa jirani, amani itaathirika.

Biashara ya kikanda barani Afrika inakabiliwa na changamoto

Licha ya idadi ya vijana bilioni 1.3 katika bara la Afrika ambayo inatarajiwa kuongezeka maradufu ifikapo mwaka 2050, biashara ya kikanda imekabiliwa na changamoto ambazo pia zilizungumziwa katika mjadala huo wa jana.

Odinga alisema kuwa Afrika ina soko kubwa la ndani ambalo inaweza kulitumia kwa mageuzi ya kiuchumi kwa kufungua fursa za biashara kati ya nchi za Afrika.

Mugabe achangia Umoja wa Afrika dola milioni moja

Youssouf alipendekeza mfumo wa malipo ya fidia ambao utahakikisha nchi hazipati hasara wakati zinafanya biashara kwa kutumia sarafu tofauti na kuongeza kuwa hakuna sababu ya kutokuwa na sarafu moja.

Randriamandrato naye, alisema kuwa miungano ya kibiashara ya kikanda kama soko la pamoja la mashariki na kusini mwa Afrika ina jukumu kubwa la kutekeleza kurahisisha biashara baina ya mataifa ya Afrika.

Umoja wa Afrikauna mapendekezo kadhaa ya marekebisho ya mfumo wake na

uongozi yanayolenga kuafikia malengo yake na wagombea wote waliahidi kutekeleza mageuzi hayo ikiwa watachaguliwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW