Wagombea wa upinzani Kongo kufanya maandamano
24 Desemba 2023Kulingana na barua hiyo ya Desemba 22 iliyotumwa kwa gavana huyo na kuchapishwa katika mtandao wa kijamii wa X na Jean- Marc Kabunda, muakilishi wa mgombea Martin Fayulu, wagombea watano wa upinzani wanapanga maandamano ya pamoja katika mji mkuu mnamo Desemba 27.
Soma pia:Matokeo ya uchaguzi wa rais Kongo kuanza kutangazwa
Barua hiyo imesema kuwa wataandamana kulalamika kuhusu kasoro zilizogunduliwa wakati wa shughuli ya kupiga kura na kabla ya kura hiyo.
Barua hiyo imeendelea kusema kuwa wataandamana dhidi ya kuongezwa kwa muda wa kupiga kura.
Tume ya uchaguzi CENI yakiri kuhusu ucheleweshwaji wa kura
Tume ya uchaguzi ya nchini humo, CENI imekiri kwamba kulikuwa na ucheleweshaji siku hiyo ya kura ambao unamaanisha kuwa baadhi ya vituo vilishindwa kufunguliwa, lakini imekataa madai kuwa uadilifu katika mchakato huo wa uchaguzi ulivurugwa kwa kuongeza muda wa upigaji kura.
Matokeo kamili ya awali ya uchaguzi huo yanatarajiwa kufikia Desemba 31.