1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagonjwa 171 wa mpox wakutwa na mpox Burundi

22 Agosti 2024

Wizara ya afya nchini Burundi imesema wagonjwa 171 wamekutwa na homa ya nyani.

DR Kongo | Mlipuko wa Mpox
Ugonjwa wa Mpox umekuwa ukienea kwa kasi katika mataifa ya Afrika.Picha: Moses Sawasawa/AP/dpa/picture alliance

Tangazo hilo linafuatia kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuthibitishwa nchini humo mwezi uliopita.

Waziri wa afya Polycarpe Ndayikeza ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, hadi sasa hakuna vifo vyovyote vilivyoripotiwa kutokana na ugonjwa huo.

Mwishoni mwa mwezi Julai, wagonjwa watatu walikutwa na mpox nchini Burundi huku wizara ya afya ikithibitisha wagonjwa wengine 153 waliokutwa na virusi vya homa ya mnamo mnamo Agosti 18.

Chanjo ya ugonjwa wa Homa ya Nyani imepatikana

00:49

This browser does not support the video element.

Soma pia: Burundi yarekodi visa vya kwanza vya mpox

Wizara hiyo imetahadharisha kuwa ugonjwa wa mpox unaendelea kuenea kwa kasi na kwamba imeanzisha mchakato wa kuweka wodi maalum katika hospitali za wilaya ili kushughulikia wagonjwa wa homa ya nyani.

Soma pia: Tanzania yaimarisha hatua za kuzuia maambukizi ya Mpox

Afisa mmoja wa afya ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wagonjwa waliokutwa na homa ya nyani wanashukiwa kuwa na aina mpya ya kirusi cha mpox kinachosambaa kwa kasi katika nchi Jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW