1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Wagonjwa watatu wa homa ya nyani wagunduliwa Pakistan

16 Agosti 2024

Pakistan imegundua wagonjwa watatu wenye virusi vya homa ya nyani.

Peru, Lima | Mpox (2022)
Picha: Ernesto Benavides/AFP/Getty Images

Taarifa hizo zimethibitishwa leo na maafisa wa wizara ya afya kwenye jimbo la kaskazini la Khyber Pakhtunkhwa.

Wizara hiyo ya afya imesema wagonjwa hao waliwasili nchini humo wakitokea Umoja wa Falme za Kiarabu.

Awali, Pakistan iliwahi kuripoti wagonjwa wa homa ya nyani japo haikubainika mara moja ni aina gani ya kirusi cha mpox kilichogunduliwa kwenye wagonjwa hao watatu.

Haya yanatokea baada ya shirika la afya duniani WHO kutangaza ugonjwa wa homa ya nyani kuwa dharura ya afya ya kimataifa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW