1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagonjwa wengine 4 wa Ebola wapona

1 Juni 2026

Wauguzi wanne waliokuwa wanatibiwa baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola wameruhusiwa kutoka hospitalini huko Bunia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

DR Kongo Goma 2026 | Ebola
Idadi ya watu waliokwisha ambukizwa nchini Kongo imefikia 282, ambapo 42 wamepoteza maishaPicha: Jospin Mwisha/AFP

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilisema kwenye taarifa yake ya Jumapili (Mei 31) kwamba wagonjwa wengine zaidi wanatazamiwa kupona, hasa pale ugunduzi na matibabu yanapoanza mapema, huku juhudi za kukabiliana na ugonjwa huo hatari zikiongezeka.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, mfanyakazi mmoja  wa maabara aliyekuwa ameambukizwa, alipona ugonjwa huo na hivyo kuifanya idadi ya waliopona kufikia watano.

Nje ya Afrika, wagonjwa wachache wanaendelea kutibiwa nchini Brazil na Italia, baada ya kupata maambukizo wakitokea mataifa yaliyokumbwa na ugonjwa huo.

Idadi ya watu waliokwisha ambukizwa nchini Kongo imefikia 282, ambapo 42 wamepoteza maisha.

WHO iliitangaza aina mpya ya kirusi cha Bundibugyo kuwa sababu ya mripuko wa sasa wa Ebola ndani ya Kongo na Uganda, ambako kumetangazwa hali ya dharura ya kiafya lakini bado haijafikia kiwango cha kuwa janga.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW