Wahadhiri na wanafunzi wa chuo kikuu cha Roma wagoma
16 Januari 2008Matangazo
ROMA:
Baba Mtakatifu Benedict amefuta ziara yake katika chuo kikuu cha Roma kufuatia maandamano ya waalimu na wanafunzi wa chuo hicho.Badala yake Baba Mtakatifu atatuma hutoba yake kwa chuo kikuu cha La Sapienza.Hakukutolewa sababu ya kufutwa kwa ziara hiyo.