1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina Austria tayari kuunda serikali na wa siasa kali

6 Januari 2025

Chama cha kihafidhina cha Austria kimesema kiko tayari kuzungumzia uundaji serikali na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, kufuatia kushindwa kukubaliana na vyama vya mrengo wa kati.

Kansela Karl Nehammer wa Austria.
Kansela Karl Nehammer wa Austria.Picha: Leonhard Foeger/REUTERS

Siku ya Jumamosi, Kansela Karl Nehammer anayeongoza chama kihafidhina cha OVP alivunja mazungumzo ya kuunda serikali bila ya chama cha siasa kali za mrengo wa kulia (FPO), ambacho ndicho kilichoshinda uchaguzi wa Septemba kwa mara ya kwanza.

Nehammer alitangaza kujiuzulu ukansela na uwenyekiti wa chama chake, na badala yake, katibu mkuu wa chama hicho, Christian Stocker, amechaguliwa kuwa kiongozi wa mpito.

Soma zaidi: Modi ajadili vita vya Ukraine na Kansela wa Austria

Stocker alisema hapo jana kwamba amepewa idhini na chama chake kuanza mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, kama akialikwa kufanya hivyo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW