1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahafidhina na mpango wa kusambaratisha serikali ya Marekani

30 Agosti 2023

Mwaka mmoja kabla ya uchaguzi wa 2024, kundi la mashirika ya kihafidhina linajiandaa kwa muhula wa pili wa Donald Trump, likiwa na mpango wa kuvunja mfumo wa sasa wa serikali a shirikisho na kutawala kwa maono ya Trump.

Washington DW I Ikulu ya Marekani, White House
Makundi ya wahafidhina yana mapngo wa kusambaratisha mfumo wa utawala wa sasa wa Marekani na kuubadilisha na maono ya Donald Trump au yanayofana nayo.Picha: Dean Pictures/IMAGO

Yakiongozwa na taasisi ya muda mrefu ya Heritage Foundation na kuchochewa na maafisa wa zamani wa utawala wa Trump, juhudi kubwa kimsingi ni serikali inayosubiri muhula wa pili wa rais huyo wa zamani, au mgombea yeyote anayelingana na maadili yao na anaeweza kumshinda Rais Joe Biden mwaka 2024.

Likiwa na kitabu cha takribani kurasa 1,000, kilichopewa jina la "Project 2025" na kile wanachokiita jeshi la Wamarekani, wazo ni kuwa na miundombinu ya kiraia kuongoza, kuunda upya na kuondokana na kile Warepublican wanakiita ukiritimba wa serikali kibaraka, kwa sehemu, kwa kuwafuta kazi wafanyakazi takribani 50,000 wa serikali ya shirikisho.

Soma pia: Timu ya kampeni ya Trump yachangisha dola milioni 7.1 baada ya picha yake kusambazwa

Tunahitaji kujaza zoni hii na wahafidhina, alisema Pual Dans, mkurugenzi wa mradi wa mpito wa urais 2025 na afisa wa zamani wa utawala wa Trump anaezungumza kwa mafanikio ya kihistoria kuhusu mkakati huo.

"Huu ni wito wa kuja Washington," alisema. "Watu wanahitaji kuweka chini zana zao, na kuachana na maisha yao ya kitaaluma na kusema, uuu ni wakati wangu wa maisha kuhudumu.

Wafuasi wa Trump walipovamia jengo la bunge la Capitol kulaazimisha wabunge kufuta matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020.Picha: JT/STAR MAX/IPx/picture alliance

Juhudi hizo zisizo kifani zinaratibiwa na mashirika mengi ya mrengo wa kulia, mengi yakiwa mapya kwa Washington, na zinawakilisha mbinu iliyobadilika ya wahafidhina, ambao kijadi wamejaribu kupunguza ukubwa wa serikali ya shirikisho kwa kukata ushuru wa shirikisho na kupunguza matumizi ya serikali.

Mpango wa wahafidhina kujaza watu wao kazini

Badala yake, wahafidhina wa enzi ya Trump wanataka kusafisha "utawala wa nchi" kutokea ndani, kwa kuwatimua wafanyakazi wa shirikisho ambao wanaamini wanazuwia ajenda ya rais na badala yao wawaweke maafisa wenye nia kama hiyo wenye hamu zaidi ya kutimiza mbinu mpya ya rais kuelekea utawala.

Lengo ni kuepusha mitego ya miaka ya kwanza ya utawala wa Trump, wakati timu ya rais wa Republican haikuwa imejiandaa vizuri, wateule wake wa Baraza la Mawaziri walipata shida kupata uthibitisho wa Seneti na sera zilipingwa na wabunge, wafanyakazi wa serikali na hata wateule wa Trump mwenyewe ambao walikataa kupindisha au kuvunja itifaki, au katika baadhi ya kesi kukiuka sheria, ili kufikia malengo yake.

Soma pia: Trump ashikiliwa na kupigwa picha ya rekodi za polisi

Wakati mengi ya mapendekezo ya mradi wa 2025 yanahamasishwa na Trump, yanaakisiwa na mahasimu wa GOP Ron DeSantis na Vivek Ramaswamy na yanapata umashuhuri miongoni mwa Warepublican.

Na ikiwa Trump atashinda muhula wa pili, kazi ya muungano wa Heritage inahakikisha rais atakuwa na watu wakuendeleza kazi ya White House ambayo haikumalizika.

"Siku ya kwanza ya rais itakuwa ngumu ya utawala wa taifa," alisema Russ Vought, afisa wa zamani wa utawala wa Trump inayeshiriki juhudi hizo ambaye kwa sasa ni rais wa taasisi ya kihafidhina ya kuifufua Marekani.

Warepublican wanaowania kuteuliwa kugombea urais wakiwa kwenye mdahalo Agosti 23, 2023. Baadhi yao pia wanaunga mawazo ya Mradi wa 2025 kuhusu kupunguza ukubwa wa serikali.Picha: Morry Gash/AP/picture alliance

'Wafanyakazi wa shirikisho siyo maadui'

Wahafidhina kwa muda mrefu wamekuwa na mtazamo mbaya wa ofisi za serikali ya shirikisho, wakilalamika kuwa zimejaa waliberali wanaokusudia kusitisha ajenda za Republican.

Lakini Doreen Greenwald, rais wa kitaifa wa Muungano wa Wafanyakazi wa Hazina ya Kitaifa, alisema wafanyakazi wengi wa shirikisho wanaishi majimbo na ni majirani zako, familia na marafiki. "Wafanyikazi wa shirikisho sio adui," alisema.

Soma pia:Joto la kiasa linaendelea kughubika Warepublican 

Ingawa marais kwa kawaida hutegemea Congress kuweka sera, mradi wa Heritage hutegemea kile ambacho wasomi wa sheria hurejelea kama mtazamo wa umoja wa mamlaka ya utendaji ambao unapendekeza kuwa rais ana mamlaka mapana ya kutenda peke yake.

Ili kuwakwepa maseneta wanaojaribu kuwazuia wateule wa rais katika Baraza la Mawaziri la urais, Mradi wa 2025 unapendekeza kuwaweka washirika wakuu kukaimu majukumu ya kiutawala, kama ilivyofanywa wakati wa utawala wa Trump ili kukwepa mchakato wa uidhinishaji wa Seneti.

Donald Trump ananipanga kuwania muhula wa pili katika uchaguzi mkuu wa 2024. Je, atafanikiwa kurejea madarakani?Picha: Butch Dill/AP/picture alliance

Ndoto za mchana kuhusu uwezo wa rais

John McEntee, afisa mwingine wa zamani wa Trump anayeshauri juhudi hizo, alisema utawala unaofuata unaweza "kucheza mpira mkali zaidi kuliko tulivyocheza na Congress."

Kimsingi Congress inaweza kushuhudia jukumu lake likipungua, kwa mfano, kwa pendekezo la kuondoa arifa ya bunge kwa baadhi ya mauzo ya silaha kwa mataifa ya kigeni.

Philip Wallach, mfanyakazi mwandamizi katika Taasisi ya Biashara ya Marekani ambaye anasoma mgawanyo wa mamlaka na hakuwa sehemu ya mradi wa Heritage, alisema kuna kiasi fulani cha "njozi" kuhusu uwezo wa rais.

Soma pia: Warepublican wavuruga kikao cha kumchunguza Trump

"Baadhi ya maono haya, yanaanza kuvuja na kugeuka mawazo ya kimabavu ambapo rais alishinda uchaguzi, kwa hiyo yeye ndiye mwenye mamlaka, hivyo kila mtu afanye anachosema, na huo sio mfumo wa serikali tunayoishi chini yake ," alisema.

Katika ofisi ya Heritage, Dans ana picha iliyofifia kwenye ukuta wake ya enzi ya awali huko Washington, na Ikulu ya White House iko karibu peke yake jijini, mitaa michafu katika pande zote. Ni taswira ya kile ambacho wahafidhina wametamani kwa muda mrefu, serikali ndogo ya shirikisho.

Viongozi duniani walaumu uvamizi wa majengo ya bunge na seneti nchini Marekani

01:59

This browser does not support the video element.

Muungano wa Urithi unapeleka juhudi zake za kuajiri barabarani, ukipita kote Marekani ili kujaza kazi za shirikisho. Waliajiri kwenye Maonyesho ya Jimbo la Iowa mwezi huu na kusajili mamia ya watu, na wanaunda hifadhidata ya waajiriwa watarajiwa, wakiwaalika kupata mafunzo katika shughuli za serikali.

"Ni kinyume," Dans alikiri - wazo la kujiunga na serikali ili kuipunguza, lakini alisema hilo ndilo somo lililopatikana kutoka nyakati za Trump kuhusu kile kinachohitajika "kupata udhibiti tena."

Chanzo: AP

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW