1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUgiriki

Wahamiaji 15 wafa baada ya ajali ya mashua Ugiriki

4 Februari 2026

Mamlaka nchini Ugiriki zinasema watu 15 wamekufa kufuatia ajali ya kugongana kwa mashua ya walinzi wa pwani ya Ugiriki na ile ya wahamiaji kando ya ufukwe wa Kisiwa cha Chios siku ya Jumanne (Februari 3).

Ugiriki Chios 2026
Watu 15 wamekufa kufuatia ajali ya kugongana kwa mashua ya walinzi wa pwani ya Ugiriki na ile ya wahamiaji kando ya ufukwe wa Kisiwa cha Chios siku ya Jumanne (Februari 3).Picha: Konstantinos Anagnostou/REUTERS

Naibu Meya wa kisiwa hicho, Pantelis Vroulis, aliiambia televisheni ya umma, ERT, kwamba miili 15 ndiyo iliyoopolewa na yote ilikuwa ya wahamiaji.

Televisheni hiyo ilitangaza kuwa watu 25 walikuwa wamepelekwa kwenye hospitali ya kisiwa hicho, 11 wakiwa watoto wadogo na wawili wakiwa maafisa wa kikosi cha ulinzi wa pwani.

Vyombo vya habari vinasema watu kadhaa walikuwamo kwenye mashua hiyo ya wahamiaji iliyokuwa ikitokea Uturuki kuelekea Kisiwa cha Chios.

Sababu ya ajali hiyo inatajwa ni pale mashua ya walinzi wa pwani ilipojaribu kuikamata mashua ya wahamiaji na kuilazimisha kugeuza njia.

Kwa mujibu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, UNHCR, kiasi cha wahamiaji 1,000 wameingia kwenye visiwa vinavyotawaliwa na Ugiriki kwenye Bahari ya Aegan wakitokea Uturuki tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW