1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiMexico

Wahamiaji 39 wafa kwa moto Mexico

28 Machi 2023

Wahamiaji 39 wamefariki dunia kwenye tukio la moto uliozuka katika kituo cha kuwazuilia wahamiaji katika mji mmoja wa Mexico unaopakana na Marekani.

Mexiko I Feuer im Gebäude des Nationalen Migrationsinstituts (INM) in Ciudad Juarez
Picha: Jose Luis Gonzalez/REUTERS

Serikali ya Mexico imesema moto huo ulizuka muda mfupi kabla ya saa sita usiku katika ofisi moja ya  taasisi ya kitaifa ya uhamiaji (INM) kwenye mji wa Ciudad Juarez na kusababisha wafanyakazi wa zima moto na magari chunguzima ya kubeba wagonjwa kukimbilia kwenye eneo hilo.

Mwandishi wa habari wa shirika la AFP amesema ameona miili chungu nzima ikiondolewa na wataalamu wa uchunguzi wa maiti  kutoka eneo la kuegesha magari la taasisi ya INM, ambapo maiti nyingine nyingi zilikuwa zimelazwa chini na kufunikwa mashuka meupe.

Mfanyakazi mmoja wa huduma ya uokozi amesema walikuweko wahamiaji kiasi 70 wengi kutokea Venezuela katika kituo kilichoteketea.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW