1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Janga

Wahamiaji 41 wapotea kufuatia ajali ya boti Mediterania

9 Agosti 2023

Wahamiaji 41 wakiwemo watoto watatu wanahofiwa kuaga dunia kufuatia ajali ya boti wiki iliyopita katika Bahari ya Mediterania; haya ni kulingana na manusura wanne waliookolewa na kufikishwa katika kisiwa cha Lampedusa.

Mittelmeer Rettungsaktion vor Lampedusa Bootsflüchtlinge
Picha: Italy Coast Guard/ROPI/picture alliance

Boti yao ya chuma ilipinduka kufuatia hali mbaya ya hewa usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa baada ya kuondoka katika bandari ya Sfax nchini Tunisia.

Manusura hao, mvulana mwenye umri wa miaka 13, mwanamke na wanaume wawili, waliokolewa na meli ya biashara na kupelekwa Lampedusa na jeshi la ulinzi wa pwani la Italia.

Wahamiaji 16 kutoka Afrika wafa maji wakiwania kuingia Ulaya

Katika taarifa tofauti, Shirika la Msalaba Mwekundu la Italia linalosimamia kituo cha kuwapokea wahamiaji kisiwani hapo, limesema wanne kati yao walikuwa katika hali nzuri kiafya. Ilithibitisha ushuhuda kuwa kulikuwa na watu 45 kwenye boti hiyo wakati ilipozama.