1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 438 waokolewa katika bahari ya Mediterania

26 Agosti 2023

Meli ya hisani inayofanya operesheni za uokoaji kwenye bahari ya Mediterania ya Ocean Vking, imewaokoa wahamiaji 438 ndani ya siku mbili zilizopita.

SOS Humanity Seenot im zentralen Mittelmeer
Picha: Danilo Campailla/SOS Humanity

Shirika linaloendesha meli hiyo la SOS Méditerranée la Ufaransa, limesema hatua hiyo ya uokozi imefanyika katika maji ya Kimataifa karibu na pwani ya Libya na Tunisia.

Siku ya Alhamisi wahamiaji 272 raia wa mataifa 23, waliokolewa kutoka kwenye boti tatu katikati ya Mediterania inayotumiwa na wahamiaji wengi dunianii wanaotaka kufika Ulaya. 

Meli ya uokozi ya Ujerumani yaokoa wahamiaji 200 Mediterania

Kati ya waliookolewa ni watoto 32 walio chini ya miaka 18 ambao hawakuwa na wazazi wao au mtu yeyote wa kuwasimamia, watoto tisa wacahanga, na watu watano walio na ulemavu. Baadae siku ya Ijumaa shirika hilo liliwaokoa watu wengine 166.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW