1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 50 wa Sudan waaga dunia Libya

17 Septemba 2025

Karibu wahamiaji 50 kutoka Sudan wamefariki dunia baada ya boti yao kushika moto katika pwani ya Libya, Jumapili.

Wahamiaji wakiwa katika boti bahari ya Medeiterenia Libya
Wahamiaji wakiwa katika boti bahari ya Medeiterenia LibyaPicha: Louisa Gouliamaki/REUTERS

Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, limesema siku ya Jumatano.

Manusura 24 wameokolewa na kuliambia shirika hilo kuwa kulikuwa na karibu watu 75 katika boti hiyo, wote wakiwa wametokea Sudan.

Chanzo cha moto huo na kituo ilipoanzia safari hiyo na kituo ilikokuwa inaelekea bado havijulikani kwa sasa.

"Hatua ya haraka inahitajika ili kusitisha majanga ya aina hiyo baharini," lilisema shirika la IOM katika taarifa.

Kulingana na takwimu za IOM, karibu watu 1,225 wamefariki dunia wakati wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterenia mwaka huu pekee.

Idadi kamili ya waliofariki lakini inatarajiwa kuwa juu zaidi kwa kuwa boti nyingi ambazo hazijasajiliwa hufanya safari zake usiku na haibainiki zinapozama.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW