1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 53 hawajulikani walipo baada ya meli kuzama Libya

Josephat Charo
9 Februari 2026

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala a uhamiaji IOM Jumatatu limesema watu 53 wamekufa au hawajulikani walipo baada ya meli kuzama katika bahari ya Mediterania karibu na pwani ya Libya.

Watu 43 wahamiaji hawajulikani waliko baada ya meli kuzama karibu na pwani ya Libya.
Watu 43 wahamiaji hawajulikani waliko baada ya meli kuzama karibu na pwani ya Libya.Picha: Pau de la Calle/AP/picture alliance

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala a uhamiaji IOM Jumatatu limesema watu 53 wamekufa au hawajulikani walipo baada ya meli kuzama katika bahari ya Mediterania karibu na pwani ya Libya.

Shirika hilo limesema katika taarifa yake kuwa meli hiyo ilipinduka kaskazini mwa Zuwara, Libya, mnamo Februari 6 na ni wanawake wawili pekee wa Nigeria waliookolewa wakati wa operesheni ya utafutaji na uokoaji iliyofanywa na mamlaka za Libya.

IOM imeongeza kwamba mmoja wa manusura alisema alipoteza mumewe na mwingine akasema alipoteza watoto wake wawili katika mkasa huo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW