Wahamiaji 56,800 wamefariki wakisafiri
1 Novemba 2018Wakati uhamiaji unaongezeka duniani, hata vifo pia vimeongezeka, hayo yamesemwa na shirika la kimataifa la uhamiaji , ambapo mamia kwa maelfu ya watu wanaofariki ama kupotea tu wakati wa kufanya safari hizo idadi imeongezeka.
Idadi kubwa ya wahamiaji wamekufa maji, wamefariki katika jangwa ama wameingia katika mikono ya wasafirishaji haramu, wakiziacha familia zao kutofahamu kile kilichowasibu.
Wakati huo huo, miili ya watu ambao hawakutambuliwa inaendelea kuzikwa kwa wingi katika makaburi katika jimbo la Gauteng nchini Afrika kusini , ama katika mji wa pwani nchini Tunisia wa Zarzis.
Makaburi kama hayo pia yanapatikana nchini Italia , Ugiriki na Libya.
Shirika la habari la Associated Press limetoa idadi ya zaidi ya wahamiaji 56,800 waliofariki ama kupotea duniani kote tangu mwaka 2014, ambayo ni karibu mara mbili ya idadi iliyopatikana katika juhudi rasmi pekee ya kuhesabu waliofariki ama kupotea iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa la shirika la kimataifa la uhamiaji.