1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUgiriki

Wahamiaji 59 wafa maji baada ya mashua yao kuzama Ugiriki

14 Juni 2023

Watu wasiopungua 78 wamekufa na dazeni kadhaa wanahofiwa kutojulikana walipo baada ya kupinduka na kisha kuzama kwa boti ya uvuvi nje ya pwani ya kusini mwa Ugiriki.

Griechenland, Kalamata | Rettungskräfte versorgen Überlebende Geflüchtete
Picha: picture alliance / ASSOCIATED PRESS

Operesheni kubwa ya utafutaji wa uokozi imeanzishwa katika eneo ilikotokea ajali hiyo, huku mamlaka zikisema watu 104 wameokolewa mpaka sasa kufuatia tukio hilo la usiku umbali wa karibu kilomita 75 kusini-magharibi mwa mkoa wa kusini mwa Ugiriki wa Peloponnese.

Kikosi cha ulinzi wa pwani cha Ugiriki  kimesema haiko wazi ni abiria wangapi hawajulikani walipo baada ya kuopolewa miili 78.

Meli sita za ulinzi wa pwani, meli moja ya jeshi la majini, ndege ya usafirishaji na helikopta ya jeshi la anga, meli kadhaa binafsi na droni kutoka wakala wa ulinzi wa mipaka wa Ulaya Frontext, zilikuwa zinashiriki katika zoezi linaloendelea la utafutaji.

Boti hiyo iliyokuwa inaelekea Italia inatajwa kung'oa nanga katika eneo la Tobruk mashariki mwa Libya.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW