1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 8 wamekufa maji wakijaribu kwenda Uingereza

Angela Mdungu
15 Septemba 2024

Takriban wahamiaji 8 wasio na nyaraka halali wamekufa mapema Jumapili 15.09.2024 katika ujia wa bahari wa kuingia Uingereza wakitokea Ufaransa. Ni baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika ujia huo wa bahari.

Wahamiaji 8 wamekufa maji wakijaribu kuvuka ujia wa bahari kutoka Ufaransa kwenda Uingereza
Watoa huduma wakiwa pembeni ya miili ya wahamiaji waliozama wakijaribu kuvuka kutoka Ufaransa kwenda Uingereza Septemba 3, 2024Picha: Denis Charlet/AFP

Mamlaka za Ufaransa zimesema boti waliyokuwemo wahamiajihao ilikuwa imejaza abiria kupita kiasi Mkasa huo umetokea wiki mbili baada boti nyingine ya wahamiaji kuzama nje kidogo ya pwani ya Ufaransa walipokuwa wakijaribu kuvuka kwenda Uingereza. Katika ajali hiyo wahamiaji wengine 12 walikufa.

Soma zaidi: Wahamiaji zaidi waingia UK kwa boti

Mamlaka za bahari za Ufaransa ziliripoti Jumamosi kuwa, wahamiaji wasio na vibali wamefanya majaribio kadhaa ya kuvuka kwa njia hiyo hatari kwa kutumia boti ndogo  ambapo watu 200 waliokolewa ndani ya saa 24 Ijumaa hadi Jumamosi wiki hii pekee.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW