Wahamiaji 80 wameokolewa, wawili wafa pwani ya Libya
18 Februari 2024Matangazo
Shirika la misaada la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF), limesema wahamiaji hao waliawaambia waokoaji kuwa wamelazimika kuogelea baada ya boti waliyokuwamo kuingia maji, ambapo wameongeza kuwa katika tukio hilo wenzao watatu walisalia katika boti hiyo na haijulikani walipo.Wahamiaji wamekua wakitumia miongoni mwa inayoelezwa kuwa ni njia hatari zaidi ulimwenguni ya uhamiaji, ya kuvuka bahari ya Mediterania wakitokea Afrika Kaskazini na kuingia Italia au Malta kwa kutumia vyombo vya usafiri visivyo salama. Ripoti iliyotolewa na Shirika la Uhamiaji, mwaka jana pekee takribani wahamiaji 2,500 waliotumia njia hiyo ya bahari walikufa au kutojulikana walipo.