Wahamiaji haramu wakufa maji nchini Ugiriki
10 Oktoba 2006Matangazo
Watu 40 hawajulikani waliko wakati meli iliokuwa ikibeba wahamiaji haramu ilipozama baharini karibu na mwambao wa kisiwa cha Kithira kusini mwa Ugiriki. Wahamiaji hao haramu ni wa kutoka Ashia.
Kuna walionusurika na kuweza kufika kwenye mwambao lakini maafisa wa serikali wanasema mvua kubwa zilizonyesha mwishoni mwa wiki zinatatiza shughuli za uokozi.
Wakati huo huo, shughuli za uchukuzi wa ndege, treni na gari kuelekea kusini zimeathiriwa na mafuriko hayo ambayo yamevikumba vijiji kiasi ya 10 na kulazimisha kuhamishwa ma mia ya watu.