1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji kurejeshwa makwao kutoka Ujerumani

Sekione Kitojo
29 Desemba 2016

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani (29.12.2016) wamejishughulisha zaidi na mjadala kuhusu kurejeshwa makwao wahamiaji, mvutano kati ya Marekani na Israel, na mpango wa kusitisha mapigano wa Urusi na Uturuki nchini Syria.

Abschiebung abgelehnter Asylbewerber nach Afghanistan - Proteste
Maandamano ya kupinga wahamiaji kurejeshwa makwao nchini UjerumaniPicha: Reuters/R. Orlowski

Tukianza na mada  kuhusu  kurejeshwa  kwa  wahamiaji ambao  maombi  yao  ya  kubakia  nchini  Ujerumani yamekataliwa , gazeti  la  Leipziger Volkszeitung linaandika:

Haijawahi  kutokea , ukamnunulia  mtu  tiketi  ya  ndege , na  kumpa kiasi  fulani cha  euro  na ukatarajia  kuonana nae tena. Matumaini  haya  yanaweza  kuwa ni  ya kufikirika  tu, wakati  nchi  anayokwenda  mtu  huyo kijiografia  iko karibu  tu  na  nchi  yako. Kugharamia  safari ya  kurejea  inawezekana  pia  kuwa  safari  ya  kurejea, yaani  huondoi uwezekano  wa  mtu  huyo  kurejea  tena. Ndio  sababu  kwa  wakati  fulani  ulazima  wa  kurejeshwa kwa  watu  kutoka  katika  mataifa  ya  eneo  la  Balkan magharibi  muda  wake umepunguzwa  mno.

Ukweli  ni  kwamba :  Utaratibu  wa  kugharamia  safari  ya kurejeshwa  nyumbani  haipaswi  kuwa  mtindo  wa kuendelezwa, anasema  hivyo  mhariri  wa  gazeti  la Braunschweiger Zeitung.

Wakimbizi wakitembea kuingia katika mipaka ya mataifa ya Umoja wa Ulaya mwanzoni mwa mwaka huu.Picha: picture-alliance/PIXSELL

Sababu  ni  kwamba  maombi  ya   hifadhi   yana  ncha nyingi. Ndio  sababu   ni  sahihi  pia , kuyaangalia  kwa kutumia  vitendea  kazi   tofauti    kutokana  na  sababu zinazotofautiana  katika  kuomba  ukimbizi. Wengi miongoni mwao , ambao  hadi  hii  leo  wanaishi  nchini  Ujerumani , walikuja  kama  wakimbizi , kwasababu  katika  mataifa  ya eneo  la  Balkan  kulikuwa  na  vita  vya  wenyewe  kwa wenyewe, kutokana  na  sababu  ya  asili  yao   ama wanakandamizwa  kutokana  na  dini  yao.

Katika  mada  kuhusu  mvutano  kati  ya  Marekani  na Israel  baada  ya  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa mataifa  kupiga  kura  katika  azimio  linaloitaka  Israel kusitisha  ujenzi  wa  makaazi  ya  walowezi  wa  Kiyahudi katika  ardhi  ya  Wapalestina, gazeti  la  Der Neue Tag linaandika.

Walowezi  karibu  400,000  wa  kiyahudi  katika   ardhi   ya Wapalestina  inayokaliwa  kimabavu   na  Israel    ya magharibi  mwa  Jordan  na  walowezi  200,000  katika eneo  la  mashariki  la  Jerusalem  ni  ushahidi  tosha , kwamba  Netanyahu  ana  lengo  moja  tu , kuzuwia  taifa la  Palestina  kuwapo  na  kuzuwia  sera  ya  mataifa  mawili kuishi  pamoja. Kwa  kuingia  madarakani  kwa  rais  mteule wa  Marekani Donald  Trump , ambae  Israel  inatarajia kupata  uungwaji  mkono   kwa  kiasi  kikubwa , amani katika  mzozo  wa  mashariki  ya  kati  haitawezekana kabisa.

Mama na watoto wake wakisubiri kuondolewa kutoka mashariki mwa Aleppo nchini SyriaPicha: Getty Images/AFP/B. Al-Halabi

Tatu Gazeti  la  Donaukurier  la  mjini  Ingolstadt  linaandika kuhusu mpango  wa  kusitisha  mapigano  nchini  Syria. Mhariri  anandika.

Kwa  wakati  huu   Vladimir Putin  ameweza  kwa  ukamilifu kutumia  mbinu  ya  kuwapo  ombwe  la  madaraka  katika Ikulu  ya  Marekani  ya  White House. Ameweza  kuchukua fursa  hiyo , kama  anavyofanya  kwa   nchi  yake  Urusi, Iran  na  Uturuki  kuhakikisha  anaamua  hali  ya  baadaye ya  Syria , bila  ya  kupata  upinzani  kutoka  Marekani. Pamoja  na  hayo  lakini  Putin  ataihitaji  hivi  karibuni Marekani.  Kuna  maslahi  makubwa  yanayoambatana  na mzozo  wa  Syria , kama  vile  Urusi  kuleta  uthabiti  katika nchi  hiyo  peke  yake.

Mwandishi:    Sekione Kitojo / inslandpresse

Mhariri: Grace Patricia Kabogo

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW