Wahamiaji vijana waunda kambi ya maandamano Paris
30 Juni 2020Dazeni kadhaa za wafanyakazi wa kujitolea kutoka shirika la Madaktari wasio na Mipaka (MSF) na mashirika mengine yasio ya kiraia walisimamisha mahema Jumatatu jioni kwenye uwanja karibu na Palace de la Republique, eneo la jadi la mikusanyiko ya maandamano mjini Paris.
Wafanyakazi hao w akujitolea wanasema wanahamiaji wanaowapigania ni watoto wa kigeni wasiokuwa na wasikindikizaji, ingawa wengi wamekataliwa maombi yao na maafisa wanaosema ni watu wazima.
"Niliwasili mjini Paris miezi saba iliyopita baada ya kupitia Libya na kutumia siku tatu kwenye boti ya mpira katika bahari ya Mediterrania kabla ya kuwasili Lampedusa," alisema Andre kutoka Ivory Coast, ambaye alisema ana umri wa miaka 17.
Lakini maafisa wa Ufaransa walisema hakuwa mtoto, uamuzi ambao aliukatia rufaa. Wakati huo huo, amekuwa akilala hotelini, shukurani kwa makundi ya misaada.
"Wamenisaidia kweli kuanzia malazi, chakula na huduma za afya," alisema Carolina Douay wa MSF, akikadiria kwamba watoto wapatao 300 wanaishi ndani au karibu na Paris.
Adha ya kusubiri kwa miezi 18
"Maafisa mjini Paris na maeneo jirani wanapaswa kutimiza wajibu wao," alisema na kuongeza kuwa, halikuwa jukumu la mashirika yasiyo ya kiserikali kufadhili huduma kama hizo.
Dazeni kadhaa za makambi zimechipuka mjini Paris katika miaka ya karibuni, zikiundwa na wahamiaji kutoka Afrika, Mashariki ya Kati na Asia Kusini, baadhi wakiwa na matumaini ya kupata hifadhi lakini wengi wengine wanakuwa na matumaini ya kufika pwani ya kaskazini karibu na Calais na hatimaye Uingereza.
Kambi nyingi zaidi zinaondolewa na polisi, na serikali imeapa kuwazuwia kufungua makaazi zaidi kwa ajili ya waomba hifadhi, ingawa imeongeza pia operesheni za kuwarejesha makwao wale ambao maombi yao yanakataliwa.
Lakini makundi ya misaada yalisema wahamiaji vijana wanaopambana kutambuliwa kama watoto wanakabiliwa na ugumu wa kusubiri hadi miezi 18.
Ayoub, kijana mwenye umri wa miaka 17 aliesema alitokea Guinea-Bissau miezi 11 iliyopita, anasema amelala baadhi ya siku katika hoteli, na siku nyingine mitaani.
Aliondoka nyumbani kwa sababu hakuweza kwenda shuleni huko, lakini amjikuta katika nafasi sawa mjini Paris. Siku hizi hafanyi "chochote", alisema, isipokuwa tu wakati anachukuwa masomo ya Kifaransa yanayotolewa na makundi ya misaada.
Chanzo: afpe