1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji wafa maji pwani ya Djibouti

2 Oktoba 2024

Watu kadhaa wanahofiwa kufa baada ya boti mbili zilizokuwa zimewabeba wahamiaji kuzama nje kidogo ya pwani ya Djibouti.

Maiti za wahamiaji kwenye ufukwe wa Djibouti.
Maiti za wahamiaji kwenye ufukwe wa Djibouti.Picha: International Organization for Migration/AP/picture alliance

Kulingana na Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa (IOM), boti hizo zilizokuwa zikitokea Yemen zilikuwa zimewabeba wahamiaji 310. 

Shirika hilo limesema hadi sasa watu 45 wamethibitishwa kufa katika tukio hilo na wengine 32 wameshaokolewa. 

Soma zaidi: Idadi ya waliofariki katika ajali ya boti Djibouti yaongezeka

Wahamiaji kutoka Ethiopia na Somalia wamekuwa wakifanya safari za hatari kupitia pwani ya Djibouti kuelekea Yemen wakijaribu kwenda Saudi Arabia na mataifa mengine ya Ghuba kwa madhumuni ya kupata maisha bora. 

Hata hivyo, mara kwa mara wahamiaji hao huishia kukwama Yemen katika mazingira hatari na magumu na hujaribu tena kurejea Djibouti.