1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani ya Kusini

Wahamiaji wapambana kuvuka mpaka wa Mexico kuingia Marekani

12 Mei 2023

Mamia ya wahamiaji wanapambana kuvuka mpaka wa Mexico na kuingia Marekani saa chache la kabla ya kuondolewa kwa vizuizi vilivyowekwa wakati wa janga la corona, vilivyowazuia wahamiaji kuomba hifadhi nchini Marekani

Mexiko Migranten in Ciudad Juarez
Picha: Andres Leighton/AP Photo/picture alliance

Kuondolewa kwa kanuni hizo kunaitishia kuongeza wimbi la wahamiaji wengi kutoka mataifa ya Amerika ya Kusini wanaovuka mpaka na kuingia Marekani kutafuta maisha bora. Mamia ya watu wameonekana wakitumia nguo kuvuka vizuizi vya seng´eng´e katika mpaka wa kusini wa Marekani licha ya onyo kutoka kwa mamlaka za nchi hiyo kwamba itawarejesha walikotoka. Afisa mmoja wa Marekani amesema idadi ya watu wanaojaribu kuingia nchini humo ilifikia 10,000 siku ya Jumanne kiwango ambacho ni maradufu ya takwimu za mwezi Machi. Hata hivyo utawala wa rais Joe Biden  tayari umeidhinisha kanuni mpya zitakazowapa nguvu maafisa usalama kuwarejesha makwao wahamiaji kabla ya kuomba hifadhi.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW