Wahamiaji wapatao 1000 wakamatwa pwani ya Libya
30 Machi 2021Hayo yameelezwa na shirika la kimataifa la kusghulikia wahamiaji IOM. Ofisi ya shirika hilo nchini Libya imesema katika kipindi cha zaidi ya saa 48 takriban wahamiaji 1000 walizuiwa na kukamatwa na kurudishwa nchini Libya na walinzi wa pwani pamoja na kikosi cha usalama wa pwani ya nchi hiyo.
Safa Msehli ambaye ni msemaji wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao yake mjini Geneva Uswizi amesema kupitia ujumbe wa Twitta kwamba waliokamatwa ni pamoja na watoto wanawake na wanaume.
soma zaidi:
Kadhalika shirika hilo limeonya kwamba wahamiaji huenda wakakabiliwa na hatua ya kuwekwa kizuizini.
Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ni njia kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterrania na wasafirishaji binadamu kwa njia za magendo wanatumia fursa ya ukosefu wa uthabiti, kufuatia kuangushwa utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moammar Kadhafi, kuimarisha shughuli zao.