Wahamiaji wapatao 50 kutoka Sudan wafariki baharini Libyahi
17 Septemba 2025
Matangazo
Manusura 24 waliookolewa, wamewaambia maafisa wa shirika hilo kuwa takriban watu 75 walikuwa ndani ya boti hiyo, wote kutoka Sudan.
Baada ya kushauriana na mamlaka nchini Libya, msemaji wa IOM amesema chanzo cha moto huo bado hakijabainika pamoja na mahali boti hiyo lilipotokea ama kukusudiwa kuelekea.
Katika taarifa, IOM imesema hatua za haraka zinahitajika kumaliza majanga hayo baharini.
Kulingana na takwimu za IOM, kufikia sasa katika kipindi cha mwaka huu, takriban watu 1,225 wamekufa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterania, ingawa idadi kamili inaaminika kuwa ya juu zaidi kwa sababu boti nyingi ambazo hazijasajiliwa hufanya safari za usiku na kukosa kutambuliwa zinapozama.