1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahanga wa Ongwen kulipwa yuro milioni 52

29 Februari 2024

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ICC imeamua kwamba karibu wahanga 50,000 wa kamanda wa Uganda Dominic Ongwen, wanastahili kufidiwa jumla ya yuro milioni 52.

uhalifu Uholanzi l Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu. Ongwen
Dominic Ongwen Picha: Sem van der Wal/Pool/ANP/picture alliance

Majaji wanesema Ongwen ambaye alikuwa mmoja wa makamanda wakuu wa waasi wa Lords Resistance Army, LRA, hana raslimali za kulipa fidia hiyo mwenyewe.

Badala yake wametaka fedha hizo zitolewe kutoka kwenye Mfuko wa Wahanga wa mahakama hiyo ambapo kila mhanga atapokea malipo ya yuro 750.

Ongwen alifunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela mwaka 2021 baada ya kupatikana na hatia katika visa 60 vya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, ikiwemo ubakaji, mauaji na utekaji nyara watoto. Kwa sasa anahudumia kifungo chake nchini Norway.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW