1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAHARIRI WA MAGATEI YA UJERUMANI WACHAMBUA LEO ZAIDI JUU YA PENDEKEZO LA WAZIRI WA NDANI OTTO SCHILY JUU YA WAKIMBIZI:

Ramadhan Ali21 Julai 2004

GAZETINI

Gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG kuhusu pendekezo hilo laandika:

"Taasisi ya kutoa hifadhi ya kisiasa kwa wakimbizi sasa inapendeklezwa ihamishiwe huko huko watokako wakimbizi.Hifadhi kwa wakimbizi haipo tena hapa ujerumani na wsala katika Umoja wa ulaya.Ikiwezekana nje ya mipaka yao mbali kabisa na wao ,mbali na ukaguzi wa vyom,bo vya kisheria vya nchi hizi na mbali na watu kujua hatima zao.

Wakimbizi wakusanywe katika kambi za wakimbizi huko huko Afrika .Hivyo bila ya kuonekana na macho ya wakaazi wa huku na asiewaona hawajui maafa yao. Kwa njia hii dhana itakuwapo kwamba kupitia mipango ya kiutawala tatizo la ufukara duniani laweza kudhibitiwa kwa hatua za kuwastusha wakimbizi hao.Kwa njia hii, neema inabakia ndani ya Ulaya, maafa na madhila yanabaki nje ya mipaka ya Ulaya. Hatua hizi zote hazitasaidia kitu kwani zinapalilia tu kuwa n a imani potofu kuwa ukiwa tajiri huhitaji kugawana na wenzako wsasio na kitu."-hilo lilikua Süddeutsche Zeitung.

Ama gazeti la TAGESZEITUNG linalotoka Berlin likiendeleza mada hii hii laandika:

"Shauri hili lililotolewa sio tangu mwanzo linakiuka haki za kimataifa bali pia si wazo jema.Kwani inafaa kuwa na shaka shaka iwapo katika jangwa la Libya kuna utaratibu wa kisheria wa kutosha kuweza kujua fulani ana haki kweli ya ukimbizi au la.Haiaaminiki kabisa kwa Umoja wa Ulaya kufaulu kuweza kuwa nao huko mawakili waliohetimu fani zao na watumishi wa kuwatunza wakimbizi.Pia haiwezi kutegemewa kuwa kwa mpango wa waziri mkuu Blair itawezekana kuzuwia uhamiaji usiodhibitiwa wakati huu.Yule atakae kuanza maisha mapya barani Ulaya ,huyo ataingia moja kwa moja katika njia za kihalifu." lamaliza gazeti.

Ama kuhusu mada nyengine ile ya majadiliano motomoto wakati huu kuhusu nyongeza za mishahara na muda wa kufanya kazi,yamehamia hata katika magazeti ya Ujerumani:

Gazeti la Munich la TZ laandika:

" Sisi ndio mabingwa wa dunia katika kuwa na muda mwingi wa mapumziko-likizo nyingi,siku kuu nyingi za mapumziko,tunafanya kazi masaa machache na hii yagharimu fedha nyingi.Kwahivyo ndio maana ingefaa kufanya kazi kama zamani masaa 40 kwa wiki au hata 50.Kutokua mkakamavu ndio hali ya wakati wetu huu.

Hali halisi ya ulimwengu wa wafanyikazi ni kutumika masaa 42 kwa wiki na mara nyingi hata kutolipwa overtime.

Mikataba ya waajiri na wafanyikazi tayari inaruhusu hivi sasa ilingane na mahitaji ya kampuni au kiwanda chenyewe kilivyo.Kuwa na mapatano jumla-jamala, muda wake umepita...."

Katika gazeti la WESTDEUTSCHEN ZEITUNG linalochapishwa mjini Düsseldorf, laandika hivi juu ya mada hii:

"Kile ambacho mameneja na hasa katika viwanda na makampuni ya ukubwa wastani wanakijua zamani,kimethibtishwa sasa na taftishi :wajerumani wanafanya kazi kwa bidii na kwa massaa mengi,kwa wastani zaidi kuliko mapatano kati ya wajiri na wafanyikazi yanavyosema.Hasa katika viwanda vidogo, kazi huwa nyingi na mara nyingi hakuna ujira kwa kufanya kazi masaa zaidi.Ingawa taftishi hii inachangia kumuruika pia ukweli wa mambo katika mjadala huu motomoto,lakini haukomeshi mjadala huo na kuumaliza.""Hilo lilikua WESTDEUTSCHEN ZEITUNG kutoka Düsseldorf.

Mwishoe, tulitupie jicho gazeti la DIE WELT ambalo limezungumzia kuchaguliwa kwa spika jana wa Bunge la Ulaya huko Strassbourg:

Gazeti laandika:

"Wingi wa wabunge wa Ulaya huko Strassbourg wanawapa haki wale ambao wiki 5 nyuma waliamua kutokwenda kupiga kura.Hili ni Bunge ambalo badala ya kumchagua spika kutoka kundi la vyama vyenye wingi Bungeni, yaani wahafidhina-limekuja kumchagua msoshalist Josep Borrell.Anatakiwa kushika wadhifa huo kwa muda wa miaka 2 kabla mhafidhina kushika madaraka hayo .Hii inatokana na kutia maanani maafikiano mengine: Maafikiano ya viongozi wa serikali ambao kwa juhudi kubwa walikubaliana mwishoe kumchagua aliekuwa waziri mkuu wa Ureno Jose Manuel Barroso kuwa rais mpya wa Tume ya Ulaya.Kwa njia hii, Bunge hili limezusha shaka shaka juu ya dhamana yake lililopewa- ambayo tangu wakati wa uchaguzi ilikwisha haribika."-

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW