1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WAHARIRI WAMEGUSIA LEO MADA TATU: KUTEULIWA KWA WAZIRI MKUU WA URENO BARROSO RAIS MPYA WA TUME YA ULAYA:MKUTANO WA KILELE WA NATO HUKO ISTANBUL NA RIPOTI YA TUME YA MABINGWA JUU YA KUIFUFUA UJERUMANI MASHARIKI.

Ramadhan Ali30 Juni 2004

GAZETINI: 30-06-04

Kuhusu kuteuliwa kwa Barroso ,gazeti la GENERAL-ANZEIGER linalotoka hapa Bonn laandika:

"Mtu barabara kwa ulaya aliestahiki wadhifa huu hakutakiwa au binafsi hakuutaka.Sasa basi, umemuangukia Jose`Manuel Durao Barroso,mreno-mjumbe wa Ulaya ambae hadi sasa hakujishughulisha sana na siasa za bara hilo.Ni rafiki wa Marekani na hivyo pia wa Uingereza.

Ni muhafidhina na hivyo kwa wakristu-wakidemokrasi wenye wingi wa viti katika Bunge la Ulaya, anaweza kutegemea kuungwamkono.Pia yeye anamtangulia Bw.Günter Verheugen (kutoka Ujerumani) ili baadae nae aweze kuwa kamishna mkuu kabisa wa UU .Ndio maana Kanzela Schröder wa Ujerumani akaungamkono kuchaguliwa Barroso."

Gazeti la MITTELBAYERISCHE ZEITUNG laandika:

"Kwao Ureno sio kuanzia pale alipoonesha ukarimu wa makaribisho ya dhati kwa wale walioungamkono vita vya Iraq kisiwani Azore alibandikwa jina la ‘mkaribishaji mwema’. Waziri mkuu huyu wa Ureno, Jose Manuel Durao Barroso ni muakilishi halisi wa tabia hii: usiwe sana na maoni yako binafsi na ukiwa nayo usieleze-bania-mpe kila mmoja haki kuwa sawa asemavyo hapo huna adui. Wakati mmoja siku za nyuma,mwanasiasa huyu mwenye umri wa miaka 48 alieparamia ngazi za juu haraka sana alikua mfuasi wa siasa za Mao-Maoist.Lakini hii ni kitambo kikubwa kilichopita na ameshavua zamani joho hilo."-lasema gazeti la MITTELBAYERISCHE ZEITUNG:

Likitugeuzia mada, gazeti la BERLINER ZEITUNG linajishughulisha na mkutano wa kilele wqa shirika la ulinzi la NATO na maazimo myake juu ya Afghanistan:

Laandika kuwa ni kwa masilahi makubwa ya Marekani na hata ya Ulaya tena haraka kuijenga dola nchini Afghanistan ambayo wakati fulani ujao kupitia nguvu zake yenyewe iweze kuzima vishindo vya waislamu wenye itikadi kali.Kuwa jukumu hili libebwe na vikosi vya kuhifadhi amani huko ni jambo walioafikiana wanachama wote wa NATO.Hatahivyo, lakini kila ikiwadia kutoa dhamana ya nani aongoze kama amirijeshi- mkuu inakua taabu kulipata dola lililo tayari kujitwika jukumu hilo.tangu mwaka sasa jukumu la ISAF limeangukia mabegani mwa shirika la NATO.

Ama gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE linatupia macho isdhara ya kisiasa kutoka mkutano huo wa kilele wa Istanbul juu ya kufunguliwa mlango wenyeji uturuki kuwa mwanachama wa UU.

Gazeti lachambua:

"Wale katika UU ambao wana shaka shaka juu ya uwanachama wa Uturuki,kwani wapo hao- na sio wachache –hawathubutu kueleza kinaga naga shaka-shaka zao hizo.

Tangu pale hoja ya kijiografia kuwa haina msingi wowote tena na tangu kuwa UU licha ya tofauti zake mbali mbali unapaswa kuwa na mafungamano mamoja ili kuwahamasisha wakaazi wake na kuwa na uwezo wa kutenda kisiasa, pingamizi zote dhidi ya Uturuki zimeporomoka.Umoja wa Ulaya ambao karibuni hivi umewafungulia mlango wanachama 10 wapya na badohaujajizatiti sawa sawa ,unajitosa katika janga jengine."

Tubadili tena mada: Kuhusu ripoti ya mabingwa juu ya kuijenga upya Ujerumani Mashariki ,gazeti la HANDELSBLATT laandika:

"Bila kujali mipaka ya mikoa inayounda shirikisho la Ujerumani,mabilioni yote ya fedha ya kuendeleza nchi hii yanapaswa tuyamimine katika yale mashina ya kiviwanda. Mikoa ambayo haina matumaini mema ya kustawi kiuchumi,serikali kuu ya shirikisho inabidi kuzuwia msaada wake kwavile haina maana kuwatwika wengine mzigo huo. Hii lakini haitakua hivyo,kwani tangu serikali kuu ya shirikisho hata za mikoa –vyama vya SPD na CDU vinawekeana pingamizi na kutiana munda---Na hiyo ndio sababu baada ya ripoti ya Tume ya kutatanisha ya DOHNANYI hakitabadilika kitu."

Tuhetimishe uchambuzi huu kwa kudondoa kutoka gazeti la STUTTGARTER NACHRICHTEN:Nalo lachambua hivi:

"Tume hiyo imechukua sasa hatua: Fedha huko Ujerumani mashariki zitolewe moja kwa moja kwa viwanda vinavyostahiki kupewa na sio tena kupitia bila faida yoyote mikononi mwa wamangi-meza.Bw.Dohnanyi na mabingwa wezake wanatumai kwa njia hii, wataibua mashina ya kustawisha uchumi.Na wazo hili ni barabara...." latumalizia uchambuzi huu STUTTGARTER NACHRICHTEN.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW