1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wanaendelea kulichambua shairi la mabishano

10 Aprili 2012

Shairi la Günter Grass na hali nchini Syria na China ni miongoni mwa mada zilizohanikiza magazetini nchini Ujerumani

Maandamano nchini SyriaPicha: Reuters

Tuanzie lakini Syria,ambako kiuna kitisho cha kushindwa juhudi za upatanishi za kimataifa.Gazeti la "Der neue Tag" linaandika:"Moscow na Beijing zitalazimika kuzindukana pindi makubaliano ya kuweka chini silaha yakishindwa.Kila siku ya ziada ya utawala wa kimabavu wa Assad,inaziangukia Urusi na China wanaomuunga mkono.Wao ndio watakao amua kwa muda gani muimla huyo ataendelea kuwasuzmbuwa wananchi wake."

Mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Lawrow na Syria Muallem (kushoto)Picha: AP

Gazeti la "Delmenhorster Kreisblatt linaonya watu wasifanye pupa.Gazeti linaendelea kuandika:"Ni Sawa kabisa kwamba jumuia ya kimataifa haipaswi kupitisha uamuzi wa haraka na kuingilia moja kwa moja kijeshi nchini Syria.Hata hivyo kuna suala linalohitaji kujibiwa nalo ni kwa muda gani tunalazimika kushuhudia maovu wanayofanyiwa raia wa kawaida na kwa muda gani wapatanishi wa kimataifa wataridhia dhihaka za Assad?Jibu la masuala hayo si rahisi kulipata.Dhahir lakini ni kwamba njia ya tahadhari watu walioamua kuifuata hadi sasa,inaangamiza maisha ya binaadam wasio wachache.

Mada yetu ya pili magazetini inatupeleka Asia ambako gazeti la "Hannoversche Allgemeine" linamuolika changamoto inayowakabili viongozi wepya katika jamhuri ya umma wa China.Gazeti linaendelea kuandika:Viongozi wepya wa China watakuwa na kazi ngumu kushinda watangulizi wao.Haitoshi tena, kama alivyofanya zamani Deng Xiaoping,kuendeleza sera za uchumi wa soko huru.Watabidi wabuni miundo mbinu kuhimiza sera hizo ziwe madhubuti.Miongoni mwa miundo mbinu ni hali ya uwazi,tangu kiuchumi mpaka kisiasaa.Na hilo hasa ndilo linalowasumbua wachina.

Mwandishi vitabu Günter GrassPicha: dapd

Shairi la mwandishi vitabu wa kijerumani Günter Grass ,alilolipa jina "Kinachobidi kusemwa" linaendelea kuchemsha vichwa vya binaadam.Serikali ya Israel imempiga marufuku kuingia nchini humo mshindi huyo wa zawadi ya uandishi sanifu ya Nobel .Gazeti la "Saarbrücker Zeitung linajiuliza:Mvutano kuhusu suala kama wasi wasi wa Grass unastahiki-kama amefanya kosa au kama amefanya makusudi kupotowa mambo,unaendelezwa kwa machungu kwasababu kinachotangulizwa mbele hapa ni tathmini ya kile kilichoandikwa.Kila mtu mwenye uwezo wa kufikiri anaweza kujipatia tathmini yake mwenyewe.Kwa kila hali lakini mzozo wa Mashariki ya kati si mzozo wa kimkoa,ni tukio linalotuhusu sisi sote.Ndio maana kila mtu ana haki ya kuingilia kati.Na Günter Grass pia....Ndio, Grass amejibwaga katika uwanja wa hatari na zaidi kuliko yote amewatonesha wafuasi wa mrengo wa kulia nchini Israel na Ulaya pia.Kama inavyodhihiriuka,onyo lake halikusaidia kitu.Lakini yajayo yatatubainishia kwa jinsi gani wasi wasi wake haukuwa na msingi."

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman