1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUhispania

Wahispania walalamika kuhusu idadi kubwa ya watalii

22 Julai 2024

Wananchi wa Uhispania wanaendelea kufadhaishwa na idadi kubwa ya watalii wanaomiminika nchini mwao. Barcelona inakusudia 'kwa kiasi kikubwa' kuongeza ushuru kwa abiria wa meli za kitalii.

Maandamano ya kupinga idadi kubwa ya watalii Barcelona
Abiria milioni 3.6 waliwasili mjini Barcelona mwaka wa 2023 kwenye meli za kitaliiPicha: Bruna Casas/REUTERS

Wananchi wa Uhispania wanaendelea kufadhaishwa na idadi kubwa ya watalii wanaomiminika nchini mwao. Barcelona inakusudia 'kwa kiasi kikubwa' kuongeza ushuru kwa abiria wa meli za kitalii ambao watakaa mjini humo kwa chini ya masaa 12. Abiria milioni 3.6 waliwasili mjini humo mwaka jana kwenye meli za kitalii. Mapema msimu huu wa kiangazi, wakaazi waliandamana kote Barcelona, wakiwamwagilia maji watalii na kuwaambia warudi makwao.

Soma pia:Watu 13 wauawa katika shambulizi la gari mjini Barcelona

Wakaazi katika maeneo mbalimbali ya Uhispania wanalalamika kuwa utalii unaongeza kodi za nyumba na gharama nyingine za maisha, na unaharibu mazingira. Wanahoji kuwa ni kundi dogo la walio wachache ambalo linavuna faida za kifedha za utalii. Wanaharakati katika kisiwa chaMallorca pia walifanya maandamano makubwa jana jioni. Nchi hiyo ya Umoja wa Ulaya ina karibu watu milioni 48. Mwaka jana, zaidi ya watu milioni 85 walitembelea Uhispania.