1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waholanzi wapiga kura kumchagua waziri mkuu mpya

22 Novemba 2023

Wapiga kura nchini Uholanzi leo wanaelekea kupiga kura katika uchaguzi wenye ushindani mkali utakaobadilisha siasa za nchi hiyo, baada ya Waziri Mkuu Mark Rutte kuweka rekodi kwa kuitawala nchi hiyo kwa miaka 13.

Siasa | Picha za wagombea katika uchaguzi Uhola
Siasa | Picha za wagombea katika uchaguzi UholanziPicha: Carl Court/Getty Images

Kura za maoni zimeonyesha matokeo tofauti kuelekea siku ya leo ya upigaji kura, huku kila mmoja wa wagombea 4 wakionekana kuwa na nafasi ya kuchukua uongozi wa nchi hiyo yenye uchumi wa tano mkubwa katika Umoja wa Ulaya.

Kura ya maoni iliyochapishwa jana ilionyesha kwambachama cha Freedom Partyambacho kinapinga Uislamu kinafungana katika uongozi na chama cha Kihafidhina cha waziri mkuu anayeondoka Mark Rutte VVD.

Soma pia: Uholanzi na Denmark kuipatia Ukraine ndege za kivita F-16

Vyama hivyo vinafuatwa kwa karibu na chama cha Leba na kile cha kijani. Suala la kuzuia uhamiaji limekuwa suala muhimu katika kampeni kwa kuwa ndilo lililochangia kusambaratika kwa baraza la mawaziri la Rutte

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW