1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi washambulia meli katika bahari ya shamu

6 Februari 2024

Waasi wa Houthi kutoka Yemen, wanaoungwa mkono na Iran, wamezishambulia meli mbili katika bahari ya shamu na kusababisha uharibifu kwa meli ya mizigo iliyokuwa ikisafiri kuelekea bandari ya Hodeidah.

Waasi wa Houthi
Kiongozi wa wahouthi Abdul Malik al- Houthi, amesema kundi lake litaendelea kushambulia iwapo Israel haitositisha vita vyake mjini GazaPicha: Indian Navy /AP/picture alliance

Serikali nchini Yemen imesema meli moja iliyokuwa ikielekea kusini mwa bahari ya shamu ilishambuliwa na ndege isiyokuwa na rubani inayoaminika kuwa ya waasi wa Houthi, hili likiwa shambulizi lao la hivi karibuni katika kampeni yao ya kushambulia meli kufuatia vita vinavyoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas katika ukanda wa Gaza.

Waasi hao wamekuwa wakishambulia meli kadhaa kwa kutumia droni na makombora katika bahari hiyo kuanzia katikati ya mwezi Novemba kwa kile walichokielezea kwamba ni kusimama pamoja na watu wa Palestina dhidi ya vita vya Israel mjini Gaza.

Iran yasema haitosita kujibu mashambulio yatakayoilenga nchi hiyo

Msemaji wa jeshi wa kundi hilo amesema wamerusha makombora katika meli mbili ya Morning Tide na Star Nasia, zilizokuwa na bendera ya visiwa vya Barbados na Marshall zinazomilikiwa na Uingereza na Marekani.

Shirika la Ambrey la usalama wa majini limesema meli iliyokuwa na bendera ya Barbados inayomilikiwa na Uingereza iliharibiwa kufuatia shambulizi hilo la angani wakati ilipokuwa ikielea kusini mashariki mwa bahari ya shamu. Ambrey imesema hakuna hata mtu mmoja aliyejeruhiwa, ikiongeza kuwa meli hiyo baadae ilibadilisha njia na kuendelea na safari zake.

Naye Mmiliki wa Meli ya Morning Tide ya kampuni ya uingereza pia ya Furadino alisema  kwa sasa meli yake inaelea bila matitizo yoyte bila kutoa maelezo zaidi. Hata hivyo Kiongozi wa wahouthi Abdul Malik al- Houthi, amesema kundi lake litaendelea kushambulia iwapo Israel haitositisha vita vyake mjini Gaza

Marekani yashutumiwa kuchochea vurugu zaidi Mashariki ya kati

Rais wa Marekani Joe Biden Picha: picture alliance / CNP/AdMedia

Huku hayo yakiarifiwa Urusi na China zimeishutumu Marekani wakati wa mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuchochea mgogoro wa Mashariki ya Kati kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi kwa makundi yanayoungwa mkono na Iran nchini Syria na Iraq.

Wahouthi wafyatua makombora kuelekea meli za kivita za Marekani

Siku ya Ijumaa jeshi la Marekani lilishambulia maeneo kadhaa katika nchi hizo mbili kama sehemu ya majibu ya mashambulizi ya droni yaliyofanyika Januari 28 katika kambi ya kijeshi ya Marekani iliyosababisha mauaji ya wanajeshi wake watatu.

Uingereza na nchi washirika washambulia maeneo ya Kihouthi Yemen

Hatua hiyo imeongeza wasiwasi kuwa vita vinavyoendelea kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas vinaweza kutanuka na kuathiri kanda nzima. Balozi wa China katika Umoja wa Mataufa Jun Zhang amesema matendo ya Marekani bila shaka yatasababisha msururu wa kulipiziana kisasi katika kanda hiyo.

Chanzo: ap/reuters

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW